Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta anaandika historia mpya katika maisha yake ya soka akiichezea club ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji, Samatta akiwa na Genk ambao inatajwa kama under dog wa Kundi E zilizopo timu za Napoli ya Italia, Liverpool ya England na RB Salzburg ya Austria.
Leo walikuwa ugenini Austria kukipiga dhidi ya RB Salzburg na kujikuta wakipoteza kwa kufungwa magoli 6-2, mtanzania Mbwana Samatta akifunga goli la pili la Genk kwa kichwa dakika ya 52 ya mchezo huo ulioshia kwa kumshundia kinda Braut Haland akipiga hart-trick.
KRC Genk sasa wana mtihani mwingine kucheza dhidi ya Napoli ya Italia katika mchezo wao wa pili wa Kundi hilo, Napoli wanaingia wakiwa na moto wametoka kumfunga Bingwa mtetezi wa michuano hiyo club ya Liverpool.
EXCLUSIVE: SAMATTA KAFUNGUKA DILI LAKE KWENDA ENGLAND, VIPI CHAMPIONS LEAGUE