Baada ya mwigizaji Shamsa Ford kuweka wazi kuwa ameachana rasmi na mume wake Chid Mapenzi miezi kadhaa iliyopita sasa ametumia ukurasa wake wa instagram kuwajuza mashabiki zake kuwa kwa sasa yupo busy na biashara zake na hana stress zozote zinazomsumbua.
Shamsa Ford amefanya hivyo baada ya kuonekana kuwa na maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii ikimuhukumu kuwa ana mawazo kutokana na issu nzima ya kuachana na mume wake hata hivyo Shamsa alienda mbali na kusema kuwa alifanya maamuzi hayo kutokana na moyo wake pamoja na akili kuridhika na ana furaha kubwa kwa sasa.
“Naomba niwachane nyie wote mnaojifanya madoctor humu insta..Hivi mm ndo wa kwanza kutoka kwenye ndoa?kwahiyo baada ya kutoka kwenye ndoa mlitegemea niwe mkiwa?nisicheze,nisifurahi hata nikicheka kwa kuonesha meno eti nina stress za kuachwa..Naomba mjue kitu kimoja am very happy with my life kwa sasa hivi sina stress hata moja zaidi ya kufikilia maisha,sanaa yangu na biashara yangu ya madera”
Mpaka nikaamua kutoka basi moyo wangu na akili yangu ililizika.Mimi siyo mwanamke ninayeweza pigana na moyo wangu kama mtu nampenda nitampigania hata iweje coz siwezi kusema HAPANA mdomoni wakati moyoni mwangu kuna NDIYO.Kwahiyo mnikomee nyie madoctor wa vichocholoni kusema mm nina stess.chochote nachofanya basi ni maamuzi yangu na ninafurahia.IAM VERY HAPPY life is too short kuangalia ya kwangu badala ya kuangalia ya kwako..G9T EVERYBODY >>>aliandika Shamsa Ford
VIDEO: BINTI AMUUA MWANAE NA KISHA KUJINYONGA ‘KILICHOFANYIKA NI KITENDO CHA KUTISHA’