Habari za Mastaa

Soudy Brown alikutana na Diamond na Zari hotelini, akatupia na swali la ujauzito #UHeard

on

ddLeo Soudy Brown ana story mtu wangu, anasema jana MARCH 26 akiwa kwenye mizunguko yake alifika katika Hoteli moja Dar, akakutana na Diamond Platnumz akiwa na mpenzi wake Zari.

Wakati huo Diamond alikuwa anakula chakula lakini Zari hakuwa anakula.. katika mazungumzo yao Soudy alimuuliza Zari kwanini yeye hali, akamjibu kwamba ameshakula sana.

Swali jingine la Soudy lilikuwa ishu ya ujauzito, akamwambia kwamba watu hawaamini kama kweli ana ujauzito.. Zari akacheka na hakujibu chochote.

Soudy aliongozana nao pia wakati wanaondoka, unaweza kusikiliza hapa mtu wangu, bonyeza play…

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments