Soudy Brown leo kapiga Stori na DJ mmoja ambae amesema kwamba staa wa Bongo Fleva, Kassim Mganga ilikuwa akafanye show Iringa lakini tayari alikuwa amepewa hela kwa ajili ya show nyingine Njombe.
Wakati wakiwa hotelini walishangaa jioni Polisi wanakuja na kumkamata Kassim baada ya kuambiwa Kassim Mganga alikuwa tayari amelipwa laki 5 na alitaka arudishiwe gharama zake ambazo zilifika zaidi ya milioni 1 lakini hakuwa nazo.
DJ huyo amesema aliamua kumdhamini Kassim ili wasimfunge, lakini baada ya hapo jamaa hakuwa anapokea simu wala hajalipa hizo pesa mpaka sasa.
Hii hapa kutoka kwenye U Heard ya Soudy Brown, ukiplay utaisikiliza yote..!!
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos