Habari za Mastaa

Ukweli wa Linex kuchukuliwa RB kisa deni la Kabati na TV upo kwa Soudy Brown… #Uheard (Audio)

on

MJEDA

Kwenye Uheard ya leo Taarifa zilizomfikia Soudy Brown ni kuhusu mfanyabiashara wa vifaa vya furniture kumchukulia RB Linex baada ya kuchukua kabati la nguo na TV tangu mwaka jana na mpaka sasa hajalipa..amesema alikwenda dukani akalipia laki sita na kuahidi baada ya wiki moja atamalizia..alichukua TV ya 700,000 na kabati la nguo la 250,000.

Amesema tayari ana RB yake na atakapokutana nae popote atamfikisha mahakamani.

Linex mwenyewe amesema ni kweli anamdai na jana alishamtumia kiasi kidogo cha pesa lakini amemlaumu kwa kudai hayo ni mambo ya kumalizana wenyewe.

Msikize hapa mfanyabiashara anayedai, Linex mwenyewe wakizungumza na Soudy Brown kwenye Uheard

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments