Habari za Mastaa

Maisha ya 50 Cent yapo hatarini, atishiwa kuchapwa risasi na polisi

on

Rapper 50 Cent ameamua kumuanika Kamanda Emanuel Gonzael kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya kuripotiwa kuwa kamanda huyo alitoa kauli kwa polisi  wenzake na kuwaambia wamchape risasi 50 Cent endapo akitokea machoni mwao.

Inaripotiwa kuwa kamanda Emanuel alitoa kauli hiyo mwezi June 2018 kwenye ‘Roll Call’ ambapo polisi walikuwa wakijiandaa kwenda kwenye mchezo wa ngumi ambao 50 Cent alipanga kuhudhuria pia hivyo Mamlaka ya usalama nchini Marekani unafanya uchunguzi kwa tuhuma za kuwaambia polisi wenzake wampige risasi 50 Cent.

Inaelezwa kuwa Kamanda Emanuel Gonzael amekuwa na bifu na 50 Cent kwa muda mrefu sasa na kuripotiwa kuwa mwezi mmoja kabla ya kutoa kauli hiyo alifungua shtaka mahakamani akidai kuwa 50 Cent amekuwa akimtishia maisha Instagram.

Imeripotiwa kuwa Rapper 50 Cent anayaweka hatarini maisha ya Gonzalez hii ni baada ya shirikisho la wafanyakazi kuibuka na kumtetea askari huyo na kudai kuwa tuhuma zote zilizotolewa na 50 Cent halina ukweli wowote na Emanuel Gonzael alisema kuwa kauli yake ya kumpiga risasi 50 Cent ilikuwa ya utani hakumaanisha.

VIDEO: ZARI NA MPENZI MPYA/ BEN KINYAIYA GUMZO/ TAARAB YA KINGEREZA

Soma na hizi

Tupia Comments