Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mwimbaji mkongwe wa RnB R.Kelly amtupia lawama aliyekuwa mke wake Andrea na kusema kuwa kutokana na uongo anaousambaza juu ya sakata lake ndio sababu inayomfanya mkongwe huyo kukosa hela za kumlipa.
Inaelezwa kuwa watu wa karibu na R.Kelly wamedai kuwa kupitia mahojiano aliyoyafanya na kituo cha TV cha CBS “This Morning” alidanganya kuhusu kukosa muda wa kuwa karibu na watoto wake inadaiwa alikuwa na miaka mingi ya kuwa nao karibu lakini alipuuzia na kusemekana kuwa tokea mwaka 2017 alikata mawasiliano na mzazi mwenzake Andrea pamoja na watoto wake watatu.
Inaripotiwa kuwa alichoongea R.Kelly juu ya watoto wake ni uongo na alitaka aonewe huruma huku taarifa nyingine zikisema kuwa alikamatwa siku ya Jumatano kutokana na kushindwa kutoa matunzo ya watoto na hivyo itagharimu kumlipa Andrea zaidi ya shilingi Milioni 378 za Kitanzania ili aachiwe huru.
MSIBA WA KIBONDE: VYAMA VYA WANAHABARI WAELEZA MAUTI ILIVYOMFIKA