Rapper 6ix9ine kutokea Marekani alimfanyia surprise mtoto mwenye umri wa miaka 8 ya kumtembelea nyumbani kwao ikiwa mtoto huyo anasumbuliwa na saratani ya ubongo.
Kitendo cha Rapper huyo kufanya hivyo ni baada ya kupokea ujumbe kupitia simu yake uliomuomba nafasi ya kukutana na mtoto huyo, Rapper 6ix9ine alikubaliana na ombi hilo na kwenda nyumbani kwa mtoto huyo ambapo anaishi siku ya Jumatatu October 22,2018.
Ndoto ya mtoto huyo ilikuwa ni kukutana na Rapper 6ix9ine na hivyo 6ix9ine alipata nafasi ya kuzunguka na mtoto huyo sehemu mbalimbali ikiwa na kumzungusha kwenye duka kubwa la nguo za watoto na kumnunulia nguo.
https://youtu.be/6Ewcklm0-EA
Nay wa Mitego kafunguka baada ya kufika BASATA “Hatuwezi kufanya kwa kubomoa”