Habari kubwa leo July 1, 2017 ni kuanza utekelezwaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 iliyopitishwa June 20 katika mfumo wa maisha ya Watanzania na uanzishwaji wa Mkoa mpya wa Kipolisi Rufiji.
Kama ulizikosa habari hizo kwenye Televisheni, Radio na Magazeti katika siku hii ya kwanza mwezi July, nimekukusanyia na kukusogezea kupitia millardayo.com.
Norway imeahidi kuisaidia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dola 10.5m (zaidi ya Tsh. 23.2b) kwa ajili ya kuboresha mamlaka hiyo. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Walimu wanaohitaji kujenga nyumba zao binafsi wameshauriwa kukopa fedha kutoka Taasisi za fedha zinazokubalika kisheria. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Kufuatia matukio ya mauaji Jeshi la Polisi limeanzisha Mkoa wa Kipolisi Rufiji ambao utakuwa chini ya aliyekuwa RPC wa Pwani, Lianga. #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
UWT imetangaza kutoa fomu za kuwania uongozi wa juu ngazi za Wilaya, Mkoa na Taifa ikisisitiza hautovumilia vitendo vya rushwa. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
UVCCM imesema Mzee Mwinyi yupo sahihi kutoa maoni binafsi baada ya kujiridhisha na utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Watu 53 wamekufa kwa ajali zilizotokea Mbeya January-June ikiwa ni pungufu ya watu 42 ya waliokufa kipindi kama hicho mwaka jana. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Wananchi wa kijiji cha Riroda, Babati wameulalamikia mradi wa maji uliogharimiwa na Bank ya Dunia kutokana na kutokidhi viwango. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Makampuni ya simu yameonywa na kutakiwa kuacha mara moja kuwalazimisha wateja wao kusikiliza matangazo yao kabla miito ya simu. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Imeelezwa kuwa ujenzi wa jengo la tatu ktk Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere unatarajia kukamilika ifikapo Sept 2018. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Shirika la Umeme (Tanesco) limezitaka kampuni zinazojishughulisha na uuzaji wa nguzo kuzingatia ubora ili waendelee na biashara. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Serikali itafanya utafiti wa kina kutumia elimu ya geomatika kubaini eneo rasmi ambalo alama ya katikati ya Tanzania inapatikana. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Waziri wa Katiba na Sheria amewasilisha miswada miwili mbele ya Kamati Maalum ya Bunge akitaka ijadiliwe kwa maslahi ya Taifa. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Spika wa Bunge Ndugai amekemea lugha na matamshi ya kuudhi yanayotolewa Bungeni na baadhi ya Wabunge akiwataka wajirekebishe. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeongeza muda wa siku 14 zaidi kwa wananchi kulipia kodi ya majengo bila adhabu hadi July 15. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Utekelezwaji wa bajeti ya Serikali 2017/18 iliyopitishwa na Bunge June 20, leo unaingia katika mfumo wa maisha ya Watanzania. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Waziri Ummy Mwalimu ameagiza kuchukuliwa hatua madaktari waliohusika sakata la mwanamke aliyedai kubiwa mtoto Hospitalini. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimesema Serikali inaandaa muswada wa sheria ya Uanasheria utakaokandamiza wanasheria. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limewaua watu sita wanaodhaniwa kuwa majambazi wilayani Kibiti usiku wa kuamkia Ijumaa. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza kushuka bei ya mafuta ukilinganisha na bei ya mwezi June. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 1, 2017
Wizara Mambo ya Ndani, IGP Sirro kuhusu mauaji ya Askari na raia wasiokuwa na hatia Kibiti, Mkuranga na Rufiji katika Mkoa wa Pwani!!!!