Top Stories

Upo single? una miaka 16+? basi hauko pabaya…

on

Hii ni kwa wale ambao bado hawajaoa au kuolewa, ni utafiti ambao umezua gumzo mitandaoni na kufanya Watu waanze kufikiria mara mbilimbili kama kilichosemwa kina uwezekano wa kutokea kwenye maisha yao.

Habari yenyewe ni kwamba utafiti uliofanywa na Journal School of Health umeeleza kwamba kama Mtu ana umri wa miaka kuanzia 16 na kuendelea basi kuna uwezekano mkubwa akawa tayari ameshakutana na Mwanamke au Mwanaume ambaye atakuja kuoana nae.

Kukutana huko hakumaanishi kwamba inatakiwa uwe umeshamfahamu bali wanamaanisha kwa mzunguko huo kuna uwezekano tayari ukawa umeshaonana nae bila nyinyi kujijua kwamba mnaweza kuja kuingia kwenye ndoa baadae.

Nukuu kutoka kwenye utafiti huo imeeleza kwamba “Inawezekana upo nae kwenye uhusiano tayari, ni Rafiki yako au huenda hamna ukaribu kwa sasa ila tambua tayari umewahi kukutana nae sehemu siku moja, ni suala la muda tu” Je hapo ulipo ukiwaza unamuona kweli kati ya wote uliokutana nao?

Soma na hizi

Tupia Comments