Premier Bet
TMDA Ad

Mix

Tatizo la Network sio Bongo pekeake, ndege hazikuruka Marekani leo !!

on

modules-Media_Gallery-gallery-Screenshots-FSX-united2

Kitaalam kuna vitu vikitokea vinasababisha network kuwa na matatizo, basi ikitokea mfano kuna tatizo kwenye network utasikia mtu analalamika eti Bongo kuna matatizo ya ajabu, hayo mambo hata Marekani yapo..!!

United Airlines walijikuta wakilazimika kuzuia safari za ndege kama 75 hivi leo July 08 2015, limetokea tatizo la network na hali ikawa mbaya kwa kama saa mbili hivi mfululizo, maelfu ya abiria ilibidi wawe wavumilivu hali ikae sawa.

NDGEE

Tumepata tatizo la mtandao asubuhi ya leo” >>> huo ndio ujumbe uliotolewa na Msemaji wa Shirika hilo, Luke Punzenberger.

united-airlines

Tatizo lilianza saa mbili asubuhi kwa saa za New York, likaisha kwenye saa nne hivi… Viwanja vingine abiria waliingia kabisa kwenye ndege lakini baada ya dharura hiyo ilibidi washuke, baada ya kila kitu kukaa sawa wakaingia tena na safari zikaanza.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments