Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha St George’s London wamegundua jinsi hisia za mapenzi zinavyoweza kumsaidia muathirika wa dawa za kulevya kupambana na hali ya arosto na kutaka kurudia matumizi ya dawa hizo iwapo aliacha kwa kipindi fulani.
Kwa mujibu wa utafiti huu binadamu huzalisha homoni inayoitwa Oxytocin ambayo humsaidia kuwa na hali ya furaha na raha ,homoni hii ambayo huzalishwa kwenye ubongo, itazalishwa kwa wingi iwapo mtu atampata mpenzi anayempenda.
Wanasayansi wanalinganisha raha na furaha anayoipata mtu akiwa na mtu ampendaye kuwa sawa na raha na furaha anayoipata mtu anayetumia dawa za kulevya kwani mtu anayetumia dawa hizo huzalisha homoni ya Oxytocin sawa na mtu aliyempata mpenzi mpya hivyo kumfanya asivute dawa za kulevya ili kuipata raha hiyo.
VIDEO: Majibu ya Harmorapa baada ya Wema Sepetu kukataa ombi lake la kuwa nae kwenye mapenzi. Bonyeza play kutazama…
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo