Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

EXCLUSIVE : “Natamani kufanya kazi na Alikiba” – Amanda

on

Amanda Swartbooi ni moja kati ya wasichana wanaotazamwa sana kwa sasa kwenye nyuso za video za wakali kutoka kwenye muziki wa Africa akionekana kwenye video za Davido ft Nasty C, Kcee wa Nigeria na Harmonize na Richie Mavoko wa Tanzania.

Kwenye exclusive interview na AyoTV Entertainment na millardayo.com Amanda Swartbooi ambaye ni raia wa Afrika Kusini amebainisha mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na historia yake kwa ufupi, kiasi cha fedha anachohitaji kufanya naye kazi pamoja na wanamuziki ambao angependa kufanya nao kazi ndani na nje ya Afrika.

“Nilipokuwa mdogo nilitamani kuja kuwa muimbaji ila najua hiyo sauti sina. Sikuwahi kuwaza nitakuja kufanya hii kazi ila nashukuru Mungu imenipa ujasiri na kujiamini zaidi kupitia kazi hii. Wazazi wangu wamekuwa wakiniunga mkono.

“Natamani kufanya kazi na Drake, lakini pia Wizkid wa Nigeria na kutoka Tanzania nigependa kufanya kazi na Alikiba.” – Amanda.

Bonyeza Play hapa chini kutazama full Interview na Amanda kutoka South Africa>>>

Video : Ilipofikia video ya Joh Makini na Davido >>>

 

Soma na hizi

Tupia Comments