Staa wa muziki wa Rap Missy Elliot ametunukiwa shahada ya uzamifu katika muziki na chuo kikuu cha Berklee College of Music Marekani pamoja na mwimbaji Justin Timberlake. Missy Elliot ambaye jina lake kamili ni Melissa Arnette Elliott ametajwa kuwa msanii wa kwanza wa kike katika muziki wa Hip Hop kutunukiwa shahada hiyo.
Missy Elliot’47 anashikilia rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa kike wa Hip Hop kutajwa kuwania tuzo ya Songwriters Hall of Fame mwaka 2019. Katika sherehe za miaka 50 ya tuzo hizo zitakazofanyika June 13, 2019 New York, Miss Elliot atakuwa msanii wa tatu kunyakua tuzo hiyo ambapo Jay Z na Jermaine Dupri tayari walifanikiwa kung’aa na tuzo ya Songwriters Hall of Fame.
Inaelezwa kuwa Missy Elliot aliwahi kuwa mtunzi kwenye baadhi ya nyimbo za Beyonce pamoja na Marehemu Whitney Houston alitamba katika tasnia ya muziki kwa takriban miaka 30 sasa na amewahi kushinda tuzo za Grammy 5. Missy Elliot alitamba na ngoma kali ikiwemo Work It, One Minute Man, Get Your Freak On na nyingine kibao.
https://youtu.be/tueAvo57mZU
VIDEO: MREMBO POSHY AMEJIBU KUDAIWA KUTOKA NA MWANAUME ANAYEDAIWA NI WA ZARI THE BOSS LADY