Moja ya stori kubwa ambayo imepewa uzito kwenye Magazeti ya Tanzania leo July 20, 2017 ni kuhusu Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kurudi tena katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kuhojiwa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Eng. Masauri amemuondoa kazini Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani ‘RTO’ Pwani Abdi Issango kwa kuzembea kutekeleza maelekezo ya Wizara.
Imeelezwa kuwa chanzo cha vurugu katika Kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM Hanang ni upangaji wa safu ya Uchaguzi Mkuu 2020. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Walimu wanaofuatilia na kutoa taarifa za wanaowakatisha masomo wanafunzi wa kike kwa kuwapa mimba, Arumeru wamelalamika kutishiwa. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Mwalimu wa Sekondari ya Francis, Kigoma amefikishwa Mahakamani akituhumiwa kumbaka mwanafunzi wa Form One mwenye miaka 14. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari Mtwara wameagizwa kutekeleza adhabu ya viboko kwa wanafunzi ili kurudisha nidhamu. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Baadhi ya walimu wastaafu wilayani Mufindi, Iringa wameiomba Serikali kuwalipa madai ya mafao yao yaliyodumu kwa miezi kadhaa. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Mkazi mmoja wa DSM Saidi Saidi (19) amehukumiwa mwaka mmoja jela kwa wizi wa mali za baba yake zenye thamani ya zaidi ya Tsh 1.3m #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
UVCCM umesema vijana wanaolalamika bila kufanya kazi, kujituma na kuchapakazi watachelewa kufikia malengo na kujikwamua kiuchumi. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Utafiti umeonesha 90% ya kinamama wanaowakata kucha watoto wao kila baada ya siku kadhaa hukosea na kuwakata na nyama za kucha. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu aliyejiuzulu Upendo Msuya amefariki dunia usiku wa kuamkia jana kutokana na ugonjwa wa kiharusi. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
"Kama unaona una ng'ombe wengi na unashindwa kuwatunza uza." – Rais Magufuli. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Rais Magufuli anatarajia kuanza ziara ya kikazi siku 3 mkoani Kigoma ambako atazindua barabara na mradi wa maji. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Watoto wa kike wameaswa kutafakari matokeo ya Kidato cha Sita mwaka huu ili kuwa chachu ya kujikinga na mimba za shuleni. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Baraza la Uuguzi na Ukunga limeagizwa kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma kusitisha leseni ya uuguzi ya Damian Mguya. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Ripoti ya tathmini ya Utawala Bora iliyotolewa na APRM imebaini Tanzania inapaswa kuboresha sekta za elimu, miundombinu, afya #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Rais Magufuli ametoa siku 14 wamiliki wa vituo vya mafuta wafunge na kutumia mashine za EFDs vinginevyo watafutiwa leseni. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Mbunge wa Singida Mashariki Lissu jana aligoma kutoka Mahakamani Dodoma kwa zaidi ya saa mbili akihofia kukamatwa na Polisi. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Serikali imeahidi kumchukulia hatua za kisheria yeyote atakayejaribu kuvuruga amani iliyopo bila kujali cheo na nafasi yake. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Mashinji na viongozi wenzake wanane wamefikishwa Mahakamani wakikabiliwa na mashtaka mawili. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Kesi ya kuomba, kupokea rushwa kupitia akaunti ya Escrow inayomkabili Meneja Misamaha wa zamani wa TRA Mutabingwa kusikilizwa Aug 17 #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Watu wawili wamefikishwa Mahakamani kwa kesi ya uhujumu uchumi wa Tsh. 12.6 kwa utolewaji wa makontena 329 bandarini bila kulipa kodi #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Undani wa kuhojiwa Waziri Mkuu wa zamani Lowassa unatarajia kufahamika leo ktk Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Serikali imesisitiza kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa na kufuatilia kwa karibu vitendo vanavyoashiria rushwa, utakatishaji fedha. #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Eng. Masauni amemuondoa kazini RTO Pwani Abdi Issango kwa kuzembea kutekeleza maelekezo ya Wizara. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Viongozi wa dini wametakiwa kuendelea kuwakemea viongozi wa kisiasa ambao wanatoa matamko ya matusi na kejeli dhidi ya serikali. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
Mfanyabiashara Yusuf Manji ambaye anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi alishindwa kufika Mahakamani kutokana na kuumwa. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 20, 2017
FULL VIDEO: Tamko la Rais Magufuli Kagera na mbinu mpya aliyowapa watu…PLAY kwenye VIDEO hii kutazama!!!
Onyo lililotolewa na Serikali baada ya watu kuendelea kuvujisha taarifa za siri!!