AyoTV

VIDEO: DR Leaky akimueleza Samatta sababu za Waingereza kupenda goli lake vs Liverpool

on

Mchambuzi wa soka mkongwe Tanzania Dr Leaky Abdallah baada ya kukutana na nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Samatta amekuja kuungana na Taifa Stars kwa ajili ya game dhidi ya Equatorial Guinea.

“Kwanza umemparamia yule kwanza sikutegemea wewe na kilo zako 50 mimi sikutegemea kama unaweza kumparamia mtu, kwani unafikiri kwa nini waingereza walipenda lile goli kwa sababu ulivyomparamia mtu (Milner)alikuwa Milner kumbe ulimparamia mkongwe yule kifaru”>>>DR Leaky

Tanzania imepangwa Kundi J katika michezo ya kuwania kucheza fainali za AFCON 2021, Kundi J lina timu za Tunisia, Equatorial Guinea na Libya na Tanzania ataanza kampeni yake dhidi ya Equatorial Guinea November 15 2019 jijini Dar es Salaam na November 19 2019 atakuwa Tunisia kucheza dhidi ya Libya.

VIDEO: SAMATTA BAADA YA KUTUA TANZANIA “HAKUNA NINACHOJUA KUHUSU EQUATORIAL GUINEA”

Soma na hizi

Tupia Comments