Ni DC Jokate Mwegelo ambae anaingia katika vichwa vya habari Wilayani Kisarawe baada ya kusimamia ujenzi wa Shule ya kwanza ya kihistoria ya wasichana ambayo imeshakamilika.
.
Sasa Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo ndie alifanya ukaguzi wa ujenzi huo wa madarasa pamoja na mabweni, nyumba za walimu, maabara kisha kupendekeza iitwae ‘Jokate Mwegelo Girls Secondary School’
.
Sasa baada ya agizo hilo la Waziri kisha Jokate kupitia twitter ameyaandika haya
Nilipoteuliwa wapo walibeza na wengine kujaribu kunivua utu wangu niliwaelewa lakini, Pwani wanasema Aso mtu hana Mungu.namshukuru Mungu wangu kwa kunitetea’- Jokate Mwegelo
.
Mh Waziri Jafo kumuelekeza DED kuisajili hii shule ya kihistoria Kisarawe iitwae Jokate Mwegelo Secondary School’- Jokate Mwegelo