Majimbo mawili ya Rushoto mkoani Tanga pamoja na lile la Ulanga mashariki mkoani Morogoro kesho November 22 yatakuwa katika uchaguzi wa kuwachagua wabunge watakao wawakilisha kwenye bunge la 11 la jamuhuri ya muungano wa Tanzania , hii ni baada ya wagombea wa majimbo hayo kufariki kabla ya uchaguzi mkuu uliofanyika October 25.
Kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC uchaguzi wa nafasi ya mbunge katika jimbo husika utalazimika kurudiwa endapo mmoja kati ya wagombea atafariki kabla ya uchaguzi kufanyika.
Hapa kaimu mkurugezi wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe ametoa ratiba nzima na taratibu za kufuata kwa wapiga kura wote>>>
“Vituo vitafunguliwa saa 1 kamili asubuhi na kufungwa saa 10 kamili za jioni, iwapo wakati wa kufunga kituo kukawa na watu waliokatika foleni na walifika kabla ya saa 10 watapata nafasi ya kupiga kura”
Baada ya kupiga kura taratibu gani itafuata? Kalieleza na hili>>
“Matokeo yote yakishapokelewa na msimamizi wa uchaguzi yatajumlishwa mbele ya mawakala na watu wote wanaoruhusiwa, baada ya kuhesabu kura fomu zitatiwa saini na mawakala watakaokuwepo.”
Hapa nimekuwekea sauti yake unaweza kuisikiliza>>>
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE