Leo April 23 2017 hukumu ya mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara imetangazwa rasmi na kamati ya maadili ya TFF, baada ya mtuhumiwa Haji Manara kushindwa kufika katika kamati ya maadili kujieleza kwa madai amepata dharura na kusafiri kwenda Zanzibar katika matatizo ya kifamilia.
Manara wa Simba aliitwa na kamati ya maadili ya TFF kwa tuhuma za makosa matatu ambayo yote ndio adhabu zake zimetangazwa na makamu mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya TFF wakili Jerome Msemwa, msemaji wa Simba aliyatenda makosa hayo April 19 katika mkutano na waandishi wa habari.
VIDEO: Kama ulikosa press ya Manara iliyofanya afungiwe miezi 12 na faini ya Tsh Milioni 9