Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka Wabunifu na Wavumbuzi wa Sayansi na Teknoloijia kwenda BRELA kusajili bunifu zao ili kuzipa Ulinzi na kulindwa kisheria.
Aidha BRELA pia imewataka wabunifu hao kurasimisha Biashara zao ili waingie katika mfumo rasmi wa kutambulika Kitaifa na Kimataifa.
Hayo yamesemwa na Afisa Utumishi na Utawala anayehusika na maombi ya Ataza, alama za Biashara na huduma BRELA Raphael Mtalima katika maonesho ya Mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Bunifu (MAKISATU) yanayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Jijini hapa.
“Niwatake hawa wabunifu na wavumbuzi walinde vumbuzi zao kwa kuzisajili BRELA, hii itamsaidia kutambulika ndani na nje hata akiitaji mkopo kwa ajili ya kuendeleza Biashara yake inakuwa rahisi”, Afisa Mtalima.
Aidha Mtalima aliongeza kuwa vumbuzi,Bunifu na teknolojia mbalimbali za Kisayansi Brela ndio Taasisi inayosismamia Sheria ya Ataza, alama za Biashara na huduma hivyo inawajibu wa kutoa kwa wajasiriamali.
“Ni lazima wabunifu hawa wafaidike na Bunifu zao kwani wanatumia pesa nyingi kufanya tafiti zao hivyo ili kuweka Ulinzi wa hizo Bunifu zao ikiwa ni njia Kuu za kuwafaidisha kisheria” Mtalima.
Aidha Afisa huyo wa BRELA pia amewataka wakazi wa Dodoma na Vitongoji vyake kutumia maonesho hayo kwenda kusajili Biashara zao kwani huduma zinapatikana hapohapo Uwanjani.
Vilevile Mtalima alisema kuwa huduma za Brela pia zinapatikana kwa njia ya mtandao hivyo popote Tanzania huduma hizo zinapatikana.
Mashindano na maonesho hayo ya MAKISATU yaliyoanza Mei 6 hadi 11 mwaka huu na yamejumuisha zaidi ya wabunifu 100.