Mix

Wafahamu Wabunge wapya walioteuliwa na NEC

on

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania ulifanyika huku baadhi ya majimbo ya uchaguzi, uchaguzi uliahirishwa kutokana na kuwepo kwa sababu mbalimbali. Tume ya Uchaguzi iliteua jumla ya Wabunge wanawake wa viti maalum 110 kati ya 113 ambapo viti vitatu vilibakizwa kusubiri uchaguzi wa majimbo nane ambayo uchaguzi wake uliahirishwa.

Chama cha Mapinduzi ‘CCM’, Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ na Chama cha Wananchi ‘CUF’ ndivyo vimetajwa kuendelea kuhusishwa kwenye mchakato wa kugawanywa viti 3 vilivyobaki kutokana na kupata angalau asilimia 5 ya kura halali za ubunge.

Leo March 24 2016 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ‘NEC’ imewateua Ritha Enespher Kabati na Oliver Daniel Semuguruka wa Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ na Lucy Fidelis Owenya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ kuwa wabunge Wanawake wa viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uteuzi huo umefuata mtiririko wa orodha iliyowasilishwa na katibu wa Chama husika ambapo CCM iliwasilisha majina nambari 65 na 66

65.Ritha Enespher Kabati

66.Oliver Daniel Semuguruka

Katika Orodha iliyowasilishwa na CHADEMA jina nambari 37

37. Lucy Fidelis Owenya

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayokwenye Twitter,FBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments