Raia wawili wa China, Zheng Rongman(50) na Ou Ya(47), wamehukumiwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu, kulipa faini ya Sh.Mil 1 kwa kila mmoja baada ya kukiri makosa ya kutoa rushwa.
Pia mahakama hiyo imetaifisha fedha kiasi cha Sh.Mil 11.5 walizotaka kutoa kama rushwa kuwa Mali ya Serikali.
Rongman ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ronglan International Industry and Trade Co. Ltd na Ya, wamehukumiwa kulipa faini na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakamani, Huruma Shaidi.
Katika hukumu hiyo, Hakimu Shaidi, alisema washtakiwa wametiwa hatiani kama walivyoshtakiwa.
Mahakama hii inawahuku kila mmoja kulipa faini ya Sh 1milioni na kiasi cha Dola za Kimarekani 5,000 ambacho ni sawa na Sh.Mil 11.5 ambazo zimetaifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Hakimu Shaidi alisema mwekezaji wote wanatakiwa wanatakiwa wafuata sheria na taratibu zilizopo nchini, hivyo kosa walilofanya washtakiwa hao halikubaliki.
Awali, wakili anayewatetea washtakiwa hao, Steven Bwana akisaidiana na Peter Lyimo na Denis Mdoe, aliomba Mahakama iwapunguzie adhabu.
Bwana alidai kuwa washtakiwa hao ni kosa lao la kwanza na kupitia Kampuni yao, wameweza kutoa ajira kwa watanzania 100 na wana familia inayowategemea.
Akisoma maelezo ya washtakiwa, Wakili kutoka Takukuru, Ipyana Mwakatobe alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.
Alidia Februari 24, 2020, washtakiwa hao walifika Makao Makuu ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) yaliyopo Wilaya ya Ilala jijini hapa kwa ajili ya kuona na kuonana na Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Edwin Mhende.
Mwakatobe alidai siku hiyo ya tukio, saa 10:00 jioni, washtakiwa hao walionana na Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Mhende Ofisi kwake akiwa na Msaidizi wake, ambapo walimueleza kuwa wana tatizo na kodi na kwamba waliwasilisha nyaraka kadhaa wakidia kuwa wamekadiriwa kiwango kikubwa cha kodi, hivyo walimuomba Kamishna huyo atatue mgogoro huo.
Washtakiwa hao baada ya kumueleza hayo Dk Mhende, walitoa kitita cha fedha ambazo ni dola za kimarekani 5,000 na kumkabidhi Kamishna huyo, kama kishawishi ili aweze kuwasaidia katika suala lao la kodi, ambapo Kampuni yao ilipaswa kulipa kodi ya Sh 1.3bilioni.
Mwakatobe alidia kuwa Dk Mhende, alimuelekeza Msaidizi wake kuzihesabu fedha hizo alizopewa na washtakiwa hao na kubaini kuwa zilikuwa ni dola.za kimarekani 5,000 , ambazo ni noti 50 za dola mia moja kila mmoja.
SUGU APASUA JIPU “DR. BASHIRU AMENIPIGIA SIMU, HII SIO SURA YA CCM WANACHUKUA WAJINGA”