Baada yakuwepo wa mgogoro katika kata ya KIA wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kuhusu kuondoka kwa wananchi kwa madai yakuwa katika eneo la uwanja wa KIA,leo hii wananchi hao wameiomba serikali kuingilia kati jambo hilo kwa kuwa vijiji hivyo vimesajiliwa kisheria nakumuomba Rais Samia kuingilia kati.
Kauli hiyo imekuja baada ya mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe kuuliza swali bungeni kuhusu hatma ya wanachi hao ikiwemo baadhi ya maeneo kurudi kwa wananchi ambapo naibu waziri wa ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara aliahidi kwenda eneo hilo kwa lengo lakumaliza mgogoro huo.