Huu ni wimbo ulioimbwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa Hip Hop kwa Tanzania,maalum kama sehemu ya harakati za kupigania kutambuliwa kwenye katiba ya nchi kama mojawapo ya kundi muhimu kwenye jamii.
Miongoni mwa makundi hayo ni kama makundi ya wavuvi,wakulima,wafugaji na wafanyakazi katika rasimu ya katiba na kuelekeza kuhusu muhimu wa ulinzi wa mali za ubunifu, si kwa wasanii pekee bali kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Wasanii walioshiriki kwenye wimbo huu ni pamoja na Quick Rocker,January Makamba,Mchizi Mox,Godzilla,Kala Jeremiah,G nako,Nikki wa Pili,Fid Q,Joh Makini,Gosby B,Mwana Fa,Kala Pina,Sugu na wengine kibao.
Na imefanywa studio za Bongo Records na producer ni P.funk
Bonyeza play kusikiliza.