Watu saba wanaaminiwa kufariki katika shambulio la bomu llililofanywa na vikosi vya Urusi, Polisi wa Ukraine wanasema.
Maafisa wanasema shambulio dhidi ya kambi ya jeshi ya Podilsk, nje ya mji wa Odessa liliwaua watu sita na kuwajeruhi wengine saba. watu 19 hawajulikani waliko huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki katika Mariupol, waliongeza kusema.
Huku hayo yakijiri Wizara ya Ulinzi ya Urusi imenukuliwa na shirika la habari la Urusi -Interfax ikisema kuwa “Ulinzi wa anga wa vikosi vya jeshi la Ukraine umekandamizwa”.
Wizara inaongeza kuwa “vikosi vya mpaka vya Ukraine havikupinga vitengo vya Urusi”.
Hakujawa na uthibitisho huru wa madai haya.