Msanii wa muziki wa HipHop Marekani, Lil Wayne amejikuta matatani baada ya polisi kuibuka nyumbani kwa msanii huyo na kuzuia baadhi ya mali zake ikiwa ni sehemu ya hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Miami siku ya Jumanne 03 November 2015.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, polisi hao walipewa ruhusa na Mahakama husika kufanya kitendo hicho baada ya rapper huyo kutoka New Orleans kushindwa kulipa gharama za ndege binafsi aliyoikodisha kwa mkataba na Miami Signature Group... mtandao huo umeendelea kusema kuwa, rapper huyo anadaiwa kiashi cha dola milion 2 ambazo ni zaidi ya bilion 4 za Kitanzania!
Polisi hao walifika nyumbani kwa rapper huyo lakini wakazuiliwa na watu wa security getini, lakini polisi walitoa taarifa kuwa wameagizwa na Mahakama ya Miami kuzuia baadhi ya mali za msanii huyo baada ya yeye kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kimkataba na kampuni ya Signature Group, kampuni inayojihusiha na biashara ya kukodisha ndege binafsi.
Unaweza pia ukaicheki video hii hapa chini kwa taarifa zaidi juu ya deni la Lil Wayne na kampuni hiyo ya ndege.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.