Mix

Jamaa alikuwa anafanya jaribio la kuingia Ikulu ya Marekani na bunduki, kilichofuatia …

on

Mtu mmoja ameripotiwa kupigwa risasi nje ya uwanja wa Ikulu ya Marekani baada ya kukaribia kituo cha ukaguzi na bunduki na kukataa amri ya kuishusha.

Taarifa zinasema mtu huyo alipelekwa hospitali ya George Washngton University akiwa katika hali mbaya, inasemekana alipigwa risasi baada ya kukataa amri iliyotolewa mara kadhaa ya kumtaka ashushe silaha aliyokuwa nayo.

Katika tukio hilo hakuna mwingine aliyedhurika, vyanzo vya habari kutoka Serikali ya Marekani vinasema maafisa wa usalama walikuwa wakimtazama mtuhumiwa na alikuwa hajaingia ndani ya Ikulu hiyo.

Mmoja wa Afisa wa Ikulu amesema Rais Barack Obama hakuwepo White House na alipewa taarifa ya hali hiyo kwamba itatokea.

HII NDIO VIDEO YA ALIYEKUWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AKIJIBU MASWALI BUNGENI AKIWA KALEWA.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments