Jina la kocha wa Arsenal Arsene Wenger limerudi kwenye headlines baada ya chama cha soka England FA kutangaza kumuadhibu kwa kitendo cha utovu wa nidhamu kilichotokea wakati wa game ya Jumapili kati ya Arsenal vs Burnley.
FA wamemuadhibu Wenger kwa kosa la utovu wa nidhamu kwa fourth official Anthony Taylor ambapo anatuhumiwa kutumia lugha ya ukali pamoja na lugha ya matusi kwa Anthony Taylor na ndio imefanya sasa afungiwe kukaa katika benchi kwa michezo minne na faini ya pound 25,000 ambayo ni zaidi ya milioni 69 za Tanzania.
Wenger atarudi benchi baada ya mchezo wa February 11 2017 dhidi ya Hull City ambapo kitendo alichofanya Wenger kilitokea kutokana na kutofurahishwa na Burnley kupewa penati dakika za majeruhi, mechi nyingine atakazozikosa Wenger ya Southampton (FA Cup) January 28, Watford (EPL) January 31 na Chelsea (EPL) February 4.
https://youtu.be/spSuR5b_NLo
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4