Michezo

Wakati katimiza mechi 1000 leo, hizi ndio rekodi zake mbalimbali za Arsenal

on

381108_heroaKocha Arsene Wenger leo katika mchezo dhidi ya Chelsea atatimiza mechi 1,000 tangu alipoanza kuifundisha klabu hiyo ya London ya Kaskazini.

Akiwa anatimiza michezo hiyo – mtandao wa Opta unaodili na masuala ya takwimu za kimichezo umetoa ripoti ya rekodi mbali mbali za Wenger ndani ya michezo hiyo 1,000.

Takwimu zinaonyesha katika mechi 1,000 ameshinda mara 572, sare mara 235, na amepoteza mechi 192.

Ameshinda makombe matatu ya Premier League, manne ya FA Cup, na manne ya Ngao ya Hisani.

Thierry Henry ndio mchezaji aliyemfungia Wenger mabao mengi zaidi, akifunga mabao 228, wakati Patrick Vieira ndio mchezaji aliyecheza mechi nyingi chini ya Wenger, jumla ya mechi 402.

381174

Tupia Comments