Jina la Wu Yongning ni mtu maarufu sana kwenye taifa la China aliesifika sana kwa kupanda majengo marefu na kuning’inia kwa hatari zaidi, kitu ambacho sio kila mmoja anaweza kufanya hivyo.
Yongning amejizolea maelfu ya Mashabiki kwenye mtandao wa kijamii wa Weibo kutokana na video zake fupi za kutisha akiwa juu ya majengo marefu bila ya kuchukua tahadhari zozote za kiusalama.
Wasiwasi uliwaingia Mashabiki zake wakati alipoacha ku-upload video zake Novemba 2017 ambapo taarifa iliyotoka baadae kwenye Media za China, zimesema kuwa amefariki baada ya kuanguka kutoka jumba la gorofa 62 kwenye mji wa Changsha.
Vyombo vya habari China vinasema kuwa sehemu mauti yalipomkuta alikuwa akishiriki kwenye mashindano ambayo angeweza kushinda pesa nyingi.
BABU SEYA NA PAPI KOCHA WALIVYOMFATA MCHUNGAJI BAADA YA KUTOKA GEREZANI,BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
KITU JPM AMEWAAMBIA MAGEREZA LEO BAADA YA KUSAMEHE KINA BABU SEYA,BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA