Leo kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili, msanii wa filamu Wema Sepetu ilitajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu lakini haikuweza kusikilizwa kwa sababu wakili wake hakuwepo.
Kesi hiyo ilitarajiwa kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, ambapo Wakili wa Serikali, Costantine Kakula alieleza kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa mashahidi wawili.
Wakili wa utetezi, Devotha Kiangakwa upande wake alieleza kuwa anamuwakilisha Wakili Peter Kibatala ambaye anamtetea Wema na wenzake ambaye amekwenda Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kwenye kesi namba 85 ya mwaka 2016, hivyo anaomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi January 10, 2018.
Ulipitwa na hii? MAHAKAMANI: Wema Sepetu hakufanyiwa upekuzi kwenye maungo yake