Top Stories

WHO “Asilimia 99 watu wanavuta hewa chafu”

on

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa limeonya kwamba karibu kila mtu duniani anavuta hewa ambayo haikidhi viwango vya ubora na kutoa wito wa hatua zaidi kuchukuliwa kupunguza matumizi ya mafuta, yanayosababisha uchafuzi, matatizo ya kupumua na kuathiri mtiririko wa damu kwa mamilioni ya watu.

Shirika la WHO limesema vifo vinaweza kuzuilika kila mwaka ikiwa hatua stahiki zitachukuliwa.

Kutokana na tathimini ya ubora wa hali ya hewa katika miji, majiji na vijiji kote ulimwenguni ambayo imehusisha jumla ya maeneo 6,000, imeonesha kuwa asilimia 99 ya watu duniani wanavuta hewa isiyo na ubora na mara nyingi ina chembechembe zinazoweza ndani kabisa ya mapafu, kuingia kwenye mishipa na kusababisha magonjwa, NBC News iliripoti Jumanne.

Ubora wa hewa ni duni zaidi katika maeneo ya Mediterania ya Mashariki na Kusini-mashariki mwa Asia, ikifuatiwa na Afrika, taarifa ya WHO iliongeza.

“Baada ya kunusurika na janga (la UVIKO-19), ni jambo lisilokubalika kuwa bado kuna vifo milioni 7 vinavyoweza kuzuilika vikichangiwa na uchafuzi wa hewa,” alisema Dk. Maria Neira, Mkuu wa Idara ya Mazingira WHO.

Soma na hizi

Tupia Comments