Duniani

Ufahamu ugonjwa unaosasabisha vifo vingi zaidi ya UKIMWI na TB duniani

on

Shirika la Afya Duniani ‘WHO’ limetoa angalizo kuchukulliwa tahadhari zaidi kupambana na ugonjwa wa ini.

Katika ripoti yake ya kwanza ya dunia kuhusu maambukizi ya ugonjwa huo, WHO imesema idadi kubwa ya watu kufariki kutokana na ugonjwa wa ini ambao unaweza kutibika unaosababishwa na matumizi ya pombe na dawa, inaongezeka.

Ugonjwa wa ini unaaminika kupoteza maisha ya watu 1.34 million mwaka 2015, idadi sawa na ile ya waliokufa kwa TB na UKIMWI, lakini wakati vifo vitokanavyo na UKIMWI na TB vikipungua, vifo vitokanavyo na ugonjwa wa ini vinaongezeka – ambapo vimeongezeka kwa 22% tangu kuanza kwa karne hii huku zaidi ya watu 325 million ambao wameathirika na ugonjwa huo hawajui kuwa wana virusi vya ugonjwa huo.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Margaret Chan amesema: “Ugonjwa wa ini sasa ni changamoto kubwa kwa afya ya jamii ambapo inahitaji juhudi za makusudi.”

VIDEO: Wizara ya Afya yatoa tamko kuhusu ugonjwa wa ZIKA Tanzania. Bonyeza play kutazama.

Soma na hizi

Tupia Comments