Baada ya kumpiga Mtangazaji Chris Rock jukwaani katika Tuzo za Oscar weekend iliyopita, Mwigizaji Will Smith ametangaza kujiuzulu kutoka ‘The Academy of Motion Pictures Arts & Sciences” ambacho ndio Chuo kinachoandaa tuzo za filamu za Oscar.
“Ninajiuzulu uanachama katika Chuo cha Sanaa na Sayansi ya Picha na nitakubali matokeo yoyote ambayo bodi itaona yanafaa, mabadiliko huchukua muda na nimejitolea kufanya kazi ili kuhakikisha kwamba sitaruhusu tena vurugu kutokea”
Baada ya tukio zima katika Tuzo za Oscar jumapili iliyopita, Chuo hicho kilitangaza tarehe 30 March kwamba kimeanzisha kesi za kinidhamu dhidi ya Smith.
HARMONIZE AFUNGUKA BANGO LINALOONESHA AKIWA NA KAJALA ‘NIMELIPIA MILIONI 12, LITAKAA MIEZI SITA’