Habari za Mastaa

Will Smith na mke wake kuachana baada ya miaka 17 ya ndoa!? Majibu haya hapa…

on

will-and-jada-smith

Kulitokea uvumi mkuba siku ya jana na kusababisha headlines kubwa juu ya masuperstaa na wanandoa Will Smith na mke wake wa miaka 17 Jada Pinkett Smith baada ya baadhi ya mitandao kuaanza kuandika kuwa wanandoa hawa wanaachana.

Tetesi hizi zilivuma mwaka 20102012 na mwaka 2013 pia laikini Will Smith na mke wake Jada Pinkett wameamua kuliongelea hili suala kupitia mitandao ya kijamii, Will alichukuwa time na kuongea yake ya moyoni kupitia Facebook kwa kuandika…

will-smith

>>> “Katika mazingira ya kawaida huwa sijisumbui kujibu tetesi za kijinga (ni kama ugonjwa) lakini nimekerekwa na watu kunipa pole kwa sababu ambazo hazipo, basi kwa niaba ya zile tetesi zote zinazopenda kujirudia mara kwa mara naomba niseme kitu kimoja na nieleweke…Jada na mimi…HATUACHANI na wala HATUPEANI TALAKA”. <<< Will Smith.

will jada

Will Smith na mke wake pamoja na watoto wao Willow na Jaden Smith.

>>> “amekuwa mke wangu kwa miaka 17 amenizalia watoto wawili wazuri…kwangu Jada ni Malkia wa moyo wangu. Mtuache jamani!”<<<  Will Smith.

Mke wake nae alichukua time na kusema kupitia mitandao ya kijamii kuwa kama ndoa nyingi duniani hata yao huwa inapatwa na misukosuko hiyo ni kawaida kwa sababu maisha kila siku yanabadilika kwa hiyo kukitokea mabadiliko mitandao hukimbilia kusema wanaachana lakini hapana hakuna kitu kama hicho kati yao.

will jada3

>>>“Mungu amenibariki na mwanaume mzuri kimuonekano na moyo wake pia, sina sababu ya kuhangaika naiheshimu familia yangu na watoto… na kila siku naingia kulala na mwanaume mwenye mvuto mno, poleni ila nimebarikiwa sina sababu ya kuomba au kutaka kuachana naye!”<<< Jada Pinkett.

Hizi ni baadhi ya post zao kwenye Twitter na Facebook

WILL FB


PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments