Watanzania wametakiwa kuwa na utamaduni wa kupanda na kutunza miti ili kujiondoa kwenye athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayochangiwa na uharibifu wa mazingira.
Akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku ya upandaji miti, Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki, Zawadi Mbwambo amesema mabadiliko ya sasa ya hali ya hewa ni matokeo ya uharibifu wa mazingira.
“Hata mvua zinavyokuwa bila mpangilio ni matokeo ya uharibifu huo, tumeona ipo haja ya kurekebisha hilo na tunafanya kwa kupanda miti, mwaka huu tumeona tusifanye sherehe za kitaifa kinachofanyika ni kuadhimishwa kikanda kila maeneo watu wanapanda miti,‘ amesema.
Katika eneo la Kilongawima ambalo ni Ukanda wa Pwani, TFS wamepanda jumla ya miti 1000 ikiwemo Mivinje na Mikoko.