Kichanga cha miezi saba (kilichozaliwa kabla ya muda) kimeokotwa kikiwa kinaelea katika mto Kapetele katika kijiji cha Sosiot, kata ya Kericho, Kenya mwishoni mwa wiki.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa eneo hilo Elijah Korir, kichanga hicho kiliokotwa na watoto wa kiume waliokuwa wanaogelea katika mto huo, kikiwa kimefungwa kwenye mfuko wa rambo.
Moto uliowaka Bar waua watu 18 China
Korir ameeleza kuwa watoto hao mwanzoni walihisi kuwa ni paka amefungwa kwenye mfuko huo na walipojaribu kuufungua ndipo walipogundua ni mtoto baada ya kuona miguu.
GWARIDE: Lilivyokaguliwa na Amiri Jeshi Mkuu Rais Magufuli Dodoma