AyoTV

VIDEO: Wizara ya Afya imewasilisha Bungeni bajeti yake ya Bilioni 845 leo

on

Mei 11 2016 Bunge la 11 limeendelea Dodoma, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017

Akisoma hotuba hiyo Waziri Ummy Mwalimu amesema…>>>’Vipaumbele vya Wizara ni vingi lakini katika mwaka 2016/2017 tutajikita katima mambo makubwa kama kuimarisha huduma za kinfa na tiba, tutaimarisha miundombinu, ujenzi utanuzi na ukarabati wa miundombini hospitalini

Katika hotuba yangu nimezungumzia usafi wa mazingira na hasa jitihada za Rais kuweka msisitizo katika usafi wa mazingira lakini pia kutambua jitihada za Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwa kuzindua kampeni ya usafi katika mkoa wa Dar es salaam

Aidha naomba Bunge likubali na kuidhinisha makadirio ya matumizi ya Wizara pamoja na Taasisi zake yenye jumla ya Shilingi 845,112,920,056.00 kati ya fedha hizo, Shilingi 317,752,653,00.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi 527,360,267,056.00 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Unaweza kuipata yote kwenye hii video hapa chini…

ILIKUPITA HII ZAIDI YA SHILINGI TRILIONI MOJA KUTENGWA KWA AJILI YA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA?

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments