Kufuatia operation iliyofanywa na Jeshi la Polisi Kagera kwa kushirikiana na mikoa ya Geita na Kigoma kuanzia August 15 hadi September 16, 57 ya bangi yamekamatwa katika ghala la mkazi mmoja wa kijiji cha Mukatoketoke, Ngara aliyeitwa Simon Charles.
Mbele ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollom, mtuhumiwa huyo amekiri kujihusisha na biashara ya kulima na kuuza bangi na kujitetea kuwa katika biashara hiyo anashirikiana na raia wa nchi jirani ya Rwanda.
Mbali na magunia hayo kukamatwa, Kamanda Ollomi amesema wamefanikiwa kumkamata Mganga feki aliyekuwa akitoa matibabu kwa binadamu, bunduki aina ya gobole na pikipiki mbili na kusisitiza kuwa operation hiyo itakuwa endelevu ili kuhakikisha vitendo vya kihalifu vinatokomea mkoani humo.
BREAKING: Meya DSM kasitisha Mkataba Kampuni ya ukamataji Magari