Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

“Nina uhakika tunaweza kushinda Lubumbashi na kufuzu”- Kocha Simba SC

on

Baada ya game ya Simba SC dhidi ya TP Mazembe kuchezwa uwanja wa Taifa na kumalizika kwa sare ya 0-0, makocha wa timu zote mbili waliongea na waandishi wa habari kuzungumzia mchezo huo huku wengine wakiamini kuwa Simba SC kwa sare hiyo kamaliza.

Kocha wa Simba Patrick Aussems ameeleza kuwa bado hawajamaliza na nafasi wanayo ya kwenda kupindua matokeo Lubumbashi, kwani pamoja na kupata nafasi na kumiliki mpira kwa timu yake ameridhishwa na uwezo waliouonesha timu yake.

“Nimeridhishwa na kiwango cha wachezaji wangu na najivunia wao kwa sababu wameonesha kiwango kwa timu kubwa kama TP Mazembe, tulikuwa na nafasi nyingi tulistahili kufunga na tumekosa penati hivyo vitu vinatokea, ndio maana hata (Mazembe) wanafurahi wanarudi Congo na sare, wiki ijayo nina uhakika tunaweza kufunga na kufuzu na uhakika”>>> Patrick Aussems

Ukimuuliza Mwinyi Zahera ishu za Ajib kurudi Simba SC….

Soma na hizi

Tupia Comments