Samatta usiku wa May 6 kuingia May 7 2019 amefanikiwa kutangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika 2019 anayecheza soka nchini Ubelgiji, tuzo ambayo inajulikana kwa jina maarufu la Ebony Shoe Award, Samatta anakuwa mchezaji wa tatu wa KRC Genk kuwahi kutwaa tuzo hiyo.
Mchezaji wa kwanza wa KRC Genk kuwahi kutwaa tuzo hiyo ni Souleymane Oulare raia wa Guinea ambaye alishinda tuzo hiyo 1999 na Moumouni Dagano raia wa Burkinafaso aliyeshinda tuzo hiyo 2002, pamoja na hayo Samatta hadi sasa anaongoza kwa ufungaji wa magoli ya Ligi Kuu Ubelgiji akiwa amefunga magoli 23 hadi sasa.
Samatta baada ya ushindi huo ameongea na kuwashukuru wote waliowezesha yeye kushinda tuzo hiyo “Kusema ukweli nimejisikia vizuri sana sababu unajua wachezaji siku zote tunajitahidi kuwa ni misimu mizuri ili mwishoni tuweze kupata kitu kama hiki, kwa hiyo kwangu mimi imekuwa vizuri ukiangalia msimu wangu 2018/2019 nimefanya vizuri sana”
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania