Top Stories

Mwanamtindo akanyaga kamba za viatu aanguka afariki dunia jukwaani (+video)

on

Inaripotiwa kuwa Mwanamitindo wa kiume Tales Soares mwenye umri wa miaka 26 amefariki dunia baada ya kudondoka jukwaani kutokana na kukanyaga kamba za viatu wakati wa maonyesho ya mavazi ya Sao Paulo’s Fashion yaliofanyika nchini Brazil.

Watazamaji waliokuwepo kwenye maonyesho hayo walidhani kuwa ni moja ya sehemu ya maonyesho baada ya kumuona Tales Soares ameanguka chini huku baadhi ya wanamitindo walionekana kuingiwa na hofu ndipo zimamoto walipojitokeza na kumkimbiza hospitalini.

Baada ya muda mchache waandaaji wa maonyesho hayo walitoa taarifa za kifo cha mwanamitindo huyo kupitia ukurasa wa twitter bila kutoa ufafanuzi juu ya kifo chake.

“Tunapenda kutoa pole kwa familia ya Tales kwa kumpoteza kijana wao, tutatoa mchango muhimu katika kipindi hiki kigumu” waliandika.

VIDEO: Ulipitwa na hii ya mwimbaji Nandy alivyo mwagiwa pesa, Dogo janja anunua album kwa milioni mbili na laki tatu? Bonyeza PLAY hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments