Inaripotiwa kuwa Mke wa Prince Harry wa Uingereza amebahatika kujifungua mtoto wa kiume, ambapo Prince Hary amesema kuwa yeye pamoja na Mke wake Meghan Markle wanafuraha ya ajabu baada ya mtoto wao wa kwanza kuzaliwa ni hali ambayo kila mzazi lazima awe nayo.
Inaelezwa kuwa mtoto huyo amezaliwa asubuhi ya May 6, 2019 Uingereza akiwa na uzito wa Kilogram 3.2 ikiwa mtoto huyo ndio wa kwanza kwa upande wa jina bado halijawekwa wazi.
Wawili hao walifunga ndoa May 19, 2018 na harusi yao iligharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 103 na ilihudhuriwa na watu maarufu duniani.
“Najiskia furaha sana,kama ilivyo kwa kila mzazi au baba lazima afurahie na kusema kuwa hichi kiumbe ni kizuri,hichi kiumbe ni kizuri na ninafuraha” >>>Prince Harry
VIDEO: ULIPITWA NA MWIMBAJI BEN POL ALIVYOIMBA WAKATI WA KUAGA MWILI WA MAREHEMU DK. MENGI? BONYEZAPLAY HAPA CHINI KUTAZAMA MWANZO MWISHO