Club ya Yanga SC leo ilikuwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuikabili watoto wa Kinondoni club ya KMC katika muendelezo wa michezo yake ya kiporo, mchezo huo ulikuwa wa nane wa Yanga msimu ambayo ina game nyingi za viporo kwa sababu ilikuwa inacheza michuano ya kimataifa.
Yanga katika mchezo huo walipata goli dakika ya 72 kupitia kwa Mrisho Ngassa lakini mambo yalibadilika dakika za nyongeza kabla ya mchezo kuisha muamuzi Elisasii aliamuru ipigwe penati baada ya beki wa Yanga Kelvin Yondani kumchezea faulo Kabunda wa KMC na penati ikapigwa na Hillary mchezo ukaisha 1-1.
Baada ya mchezo kaimu kocha mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwassa alilalamika kuhusiana na aina yapenati iliyotolewa lakini kubwa kupangia ratiba aliyoiita mbovu kwa sababu Yanga walicheza Ijumaa na Alliance jijini Mwanza na Jumatatu wakaambiwa waje wacheze Dar es Salaam kitu ambacho anaona sio sawa.
VIDEO: PAMBANO LA ROUND 10: MWAKINYO VS TINAMPAY