Michezo

Matokeo ya Yanga vs Ruvu Shooting – Mbeya City vs Coastal Union haya hapa

on

YANGA WAKISHANGILIAMabingwa wa Tanzania bara klabu ya Dar Young Africans leo imetoa kipigo cha mbwa mwizi kwa klabu ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliochezwa uwanja wa taifa Dar es salaam.

Katika mchezo huo ulioisha hivi punde mabao ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji Didier Kavumbagu katika sekunde ya 40 ya mchezo, kabla ya Msuva kufunga bao la pili katika dakika ya pili.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda aliyeanza kuichezea Yanga leo tangu apewe ruhusa na Fifa, Emmanuel Okwi akaziona nyavu za Ruvu katika dakika ya 27, dakika 3 baadae Mrisho Ngassa akaipatia Yanga bao la 4. Hadi timu zinaenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao 4-0.

Kipindi cha pili Yanga wakarudi kwa kasi na kufanikiwa kuongezea mabao mawili yaliyofungwa na Kavumbagu tena, Hamisi Kiiza na Saimon Msuva akafunga hesabu kuhitimisha ushindi wa mabao 7-0.

Wakati huo huo timu ya Mbeya City nayo imefungwa 2-0 na Coastal Union katika mchezo uliochezwa huko Mkwakwani Tanga. Mabao ya Coastal yamefungwa na Mohamed Mtindi.

Tupia Comments