Baada ya mwimbaji Chris Brown kukamatwa mwaka jana(2018) kufuatia tukio la kumpiga ngumi mpiga picha lilitokea Tampa nightclub Marekani mwaka 2017, sasa inaripotiwa kuwa Mahakama Kuu ya mjini Florida nchini Marekani imefuta shtaka juu ya kesi hiyo.
Imeripotiwa kuwa Mahakama imefikia kuchukua maamuzi hayo juu ya mwimbaji huyo kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha kwenye kesi hiyo, hata hivyo Mahakama ilieleza kuwa May 31,2019 Chris Brown alitakiwa kuonyesha ushahidi wake na imeonekana kuwa kwa upande wa mshatakiwa hawakuwa na ushahidi wa kutosha.
Chris Brown aliwahi kukanusha shtaka hilo na kudai kuwa hakufanya kitendo hicho ambapo mpiga picha huo alidai kuajiriwa kupiga picha katika club hiyo lakini Chris Brown alionekana kupinga kile alichokuwa akifanya na kuamua kumvamia na kumpiga ngumi ya mdomo.
ULIPITWA NA HII YA RC MWANRI ‘KAAMSHE DUDE’ TEMBEZA MKONG’OTO KICHWA KILIE KAMA NGOMA YA DAKU’? (+VIDEO)