Staa wa Bongo Fleva Dogo Janja kupitia mahojiano aliyoyafanya na Willy Mtuva kwenye kipindi cha Mseto akiwa nchini Kenya siku kadhaa zilizopita amefuunguka kuhusu ndoa yake na aliyekuwa Mke wake ambae ni Irene Uwoya.
Dogo Janja amegusia ishu ya wazazi wa pande zote mbili kutoridhia ndoa aliyoifunga pamoja na Irene Uwoya na pia amekiri kuwa kuna vitu ambavyo vilikuwa vikimkwaza ndani ya ndoa yake lakini hakuwahi kumsaliti mke wake.
Janja amefunguka pia kuwa aliwahi kuumizwa ndani ya mahusiano yake ya kimapenzi mpaka kufikia hatua ya kutaka kujirusha nje ya gari.
“Nilishawahi kulizwa kwenye mapenzi kama haujawahi basi wewe sio shujaa , kisa kilikuwa kukamatwa nina-chat na mtu mwingine ilifikia hatua kwasababu nilikua nimekunywa pombe nilitaka kujirusha nje ya gari wakati linatembea lakini baadae nilikomaa mpaka naingia ndani ya ndoa” >>>Dogo Janja
VIDEO: VANESSA MDEE AKUTANA NA NGULI WA MUZIKI AFRIKA M’BILIA BEL