Mapema leo August 4, 2017 Kamanda wa Usalama Barabarani, SACP Fortunatus Musilimu amefanya ziara kushtukiza Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani Ubungo Dar es salaam na kuzindua mpango wa uwekaji namba za simu kwenye mabasi.
Namba hizo ni maalumu kwa ajili ya abiria kupiga simu endapo dereva atakiuka sheria za barabarani zinazopelekea kusababisha ajali huku pia Ayo TV na millardayo.com zikishuhudia ukaguzi wa mabasi hayo kabla ya kuondoka ambapo yalikaguliwa moja baada ya jingine.
Inspekta Ibrahim Omary ambaye aliongoza ukaguzi huo alisema:>>>”Changamoto kubwa ni kwamba magari mengi bado ni ya zamani kwa hivyo hata vifaa vyake sio imara na kwamba wamilili wa magari mara nyingi hawapewi taarifa sahihi za magari yao na makondakta na madereva endapo yana hitilafu na yanapohitaji marekebisho.” – Inspekta Ibrahim Omary.
ULIPITWA? Kamanda wa Usalama Barabarani alivyoshtukiza Ubungo Terminal Alfajiri na kuuzindua mpango huu…tazama kwenye video hii!!
Tazama kwa kuplay video hii jinsi IGP Simon Sirro alivyoshtukiza Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo na alichokifanya!!!