Mix

Dina Marios aendelea na majukumu yake ya Ubalozi hadi Shule ya Tabata

on

Jumanne hii Dina Marios ambaye ni balozi wa Star Time walitembelea shule ya Msingi Tabata iiliyoko Ilala jijini Dar es Salaam ambapo wawakilishi wa StarTimes walikutana na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la 2, 3, 4 na 5 kutoka shule hiyo.

Pamoja na kuzungumza na wanafunzi wawakilishi wa StarTimes pamoja na Dina Marios walitoa zawadi kwa ya king’amuzi na Dish kwa uongozi wa shule na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi walioweza kujibu vizuri maswali yaliyoulizwa.

“Tumepokea vizuri ugeni wa StarTimes hapa shuleni kwetu na kwa zawadi waliyotupatia. Pia wamewapatia changamoto nzuri wanafunzi wetu kwa maswali waliyowauliza.” Mwl. Mkuu wa Shule ya Msingi Tabata Bi. Rosalia P. Mrema.

ST Kids ni chaneli ya kwanza Tanzania ya watoto ambayo vipindi vyake vinapatikana kwa lugha ya Kiswahili, lengo likiwa ni kuwawezesha watoto kuburudika na katuni na maudhui mengine kwa lugha ambayo wanaifahamu vizuri ili kusaidia ukuaji wao miongoni mwa familia na jamii zao.

“Lengo letu kutembelea shule hizi ni kutambulisha maudhui mapya yanayopatikana katika chaneli ya ST Kids ambayo yako katika lugha ya Kiswahili. Vipindi ni vizuri kwa watoto kwani vinawafundisha stadi mbali mbali za maisha na pia vinaleta uhusiano mzuri baina yao na wazazi kwani wanaweza kuelezea hisia zao kupitia vipindi hivyo” Samwel Gisayi – Afisa Mahusiano, StarTimes Tanzania.

Kampeni hii ya kutembelea mashule jijini Dar es Salaam itaendelea hadi mwisho wa mwezi wa tano na itafikia jumla ya shule 7 katika Wilaya 3 za Mkoa wa Dar es Salaam.

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments