Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Mwinyi Zahera hajaichukulia poa kauli ya Haji Manara

on

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameeleza malalamiko yake kuhusiana na kauli ya msemaji wa Simba Haji Manara kuhusiana na kauli yake aliyoitoa wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu ya ujio wa Sevilla nchini Tanzania, Simba itacheza na Sevilla May 23 2019 mechi ya kirafiki.

Hivyo kuelekea mchezo huo Simba SC kupitia kwa Haji Manara aliomba kuwa anaomba TFF iwape Kombe la Ubingwa wa TPL baada ya game ya Sevilla endapo Simba SC watakuwa wamefikia point ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, Mwinyi Zahera ametafsiri kauli hiyo kama Simba SC wapo na mpango wa nyuma ya pazia.

“Ile ya kusema Manara mtupatie Kikombe wakati Sevilla atakuja si mlishajua mpango wenu jinsi ulivyo wakati Sevilla atakuja mtakuwa mmemaliza ma mechi umesikia, ile inaonekana kabisa mpango ulishakuwa tayari unafaa, mimi siiti kwamba Simba anabeba Kikombe Simba anapewa kikombe, habebi kikombe anapewa kikombe”>>>Mwinyi Zahera

CHANZO: Azam TV and Zakazazi

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments